Mimi nimejifunza mwenyewe kuandika mashairi kwa uhodari kwa lugha ya Kiingereza zaidi. Nimekuwa nikiandika mashairi kwa miaka ishirini na bado ninajifunza. Ushairi ni nyenzo kwangu ya kujifunza, kufundisha, kutatua, kutetea, na kujiburudisha. Kuna namna unaweza andika shairi kwa kufuatia mtindo wa wimbo au sanaa ya picha. Pia kuna namna unaweza kuchukua shairi la lugha nyingine na kulitafsiri jinsi unavyojua mwenyewe bila kuwa sahihi. Kutumia njia ya tafsiri, mimi binafsi hutegemea zaidi sauti ya neno nikilitamka kwa sauti.
Kwa miaka 13 sasa nimeshiriki kwenye National/Global Poetry Writing Month (Na/GloPoWriMo) ya kule Marekani kama mshiriki wa kimataifa. Mwaka huu shairi langu moja lililofuata mtindo wa muziki wa “heavy metal” lilichaguliwa shairi bora la siku. Ukitaka kulisoma bonyeza hapa.
Kuna wimbo ninausikia sana sasa hivi huko mitandaoni. Kila nikiusikiliza najikuta nataka kupiga gwaride kama enzi zangu za ukuruta kule Mgambo JKT. Ghafla nikakumbuka hata force namba yangu AKB 2322. Nimepekua mafaili yangu kumbe cheti cha JKT bado ninacho. Wewe mwenzangu uliyeenda jeshini unakumbuka kulipiga kwata? Basi karibu kulisoma shairi hili hapo chini. Nimeliweka sambamba na wimbo husika. Kile kibwagizo cha “chikichi chikichii”, “heyeyeee” au “haya haya haya” weka popote unapotaka 🙂
