Skip to main content

WoChiPoDa 2022 is coming to Tanzania with exciting news!!!

The founder and the committee of coordinators for WoChiPoDa in Tanzania are inviting children aged 7 – 12 to a poetry contest. Poems must be in either English or Kiswahili language. An adult (parent, guardian, or teacher) should send one poem entry to wochipodacompetition@gmail.com

The deadline for submission is 31 July 2022. Winners will be announced in October 2022.

Refer to the flyer for more details including the winning prizes.

The Judging Panel consists of:

Justine P. Kakoko, the host and originator of the contest, is an author, poet, literature in English teacher, and literacy specialist who is determined to foster reading and writing habits among Tanzanian children. In addition, he is the coordinator of WoChiPoDa in the Rukwa Region.

Rehema Kawambwa is a writer and has one published poetry book. She is also the coordinator of WoChiPoDa in the Pwani Region.

Eric F. Ndumbaro is an Assistant Lecturer at Mwenge Catholic University (MWECAU). Ndumbaro won two Ebrahim Hussein Poetry Awards in 2014 and 2017. He holds BA (Kiswahili) and MA (Kiswahili) degrees in 2013 and 2017, respectively, from the University of Dar es Salaam, Tanzania. As a skilled poet, he has volunteered several times to make WoChiPoDa events successful in schools.

Gloria D. Gonsalves, the founder of WoChiPoDa, is an award-winning author and multi-published poet. Her poetry has appeared in various literary magazines and journals, including being featured five times by National/Global Poetry Writing Month (NaPoWriMo/GloPoWriMo).

WoChiPoDa 2022 inakuja Tanzania na habari za kusisimua!!!

Mwanzilishi na kamati ya waratibu wa WoChiPoDa nchini Tanzania wanawaalika watoto wenye umri wa miaka 7 – 12 kwenye shindano la ushairi. Mashairi lazima yawe katika lugha ya Kiingereza au Kiswahili. Mtu mzima (mzazi, mlezi, au mwalimu) atume ingizo moja la shairi kwa wochipodacompetition@gmail.com

Mwisho wa kutuma shairi ni tarehe 31 Julai 2022. Washindi watatangazwa mwezi Oktoba 2022.

Tazama kipeperushi kwa maelezo zaidi pamoja na zawadi za ushindi.

Jopo la Majaji:

Justine P. Kakoko, mhusika mkuu na mwanzilishi wa shindano hili, ni mwandishi, mshairi, mwalimu wa fasihi ya Kiingereza, na mtaalamu wa kusoma na kuandika ambaye amedhamiria kukuza tabia ya kusoma na kuandika miongoni mwa watoto wa Kitanzania. Aidha, ni mratibu wa WoChiPoDa katika Mkoa wa Rukwa.

Rehema Kawambwa ni mwandishi na ana kitabu kimoja cha mashairi kilichochapishwa. Pia ni mratibu wa WoChiPoDa mkoani Pwani.

Eric F. Ndumbaro ni Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Ndumbaro alishinda Tuzo mbili za Ushairi za Ebrahim Hussein mwaka wa 2014 na 2017. Ana digrii za BA (Kiswahili) na MA (Kiswahili) mwaka wa 2013 na 2017 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Kama mwanashairi aliyebobea, ameshajitolea mara kadhaa katika kufanikisha hafla za WoChiPoDa mashuleni.

Gloria D. Gonsalves, mwanzilishi wa WoChiPoDa, ni mwandishi aliyeshinda tuzo ya fasihi ya watoto na mshairi aliyechapishwa kwa wingi. Ushairi wake umeonekana katika majarida mbalimbali ya fasihi, ikiwa ni pamoja na kuchaguliwa mara tano kama mfano katika Mwezi wa Kuandika Mashairi wa Kitaifa nchini Marekani.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.