Nakubali (Swahili Poem)

Usimeze maneno yako, kaka mtanashati,
Ruhusa nakupa, siku ya rehema Jumapili,
Leo nitafurahi, kusikia ya mtima wako,
Nakubali wito wako, nitamkie hisia zako.

Sogea karibu nami, nipe busu la mkono,
Haya isikukweze, nieleze yako mahaba,
Siri haina nafasi, leo miye kipenzi chako,
Nakubali wito wako, nitamkie hisia zako.

Karibu usiogope, fichua ya moyoni mwako,
Moyo wa kupenda, usiutafutie mithali,
Fariji roho yako, upendacho ndicho itakacho,
Nakubali wito wako, nitamkie hisia zako.

Pato lako leo mahaba, undani wako nionyeshe,
Penzi la kujitolea, tamu yake hushinda asali,
Najikabidhi kwako leo, nienzi kushinda halua,
Nakubali wito wako, nitamkie hisia zako.

Subira leo imeniisha, maliza kiu changu,
Niache hoi leo, kwa ndoto za mahaba,
Niandikie shairi, malizia na hariri ya sauti,
Nakubali wito wako, nitamkie hisia zako.

©Gloria D. Gonsalves

Recent Comments

 • DON SHUSHU
  July 10, 2014 - 10:24 am · Reply

  sitomeza maneno yangu,leo wazi nakutamkia,
  unauumiza moyo wangu,kila nikikufikiria,
  hupasuka moyo wangu,na machozi nikilia,
  vipi utakuwa wangu,ndio nilikuwa nikifikiria,
  leo nimepata bahati,nitakuelewa muhibu,

  na kilicho nishawishi,ni haya nyonda pulika
  ni yako macho na nyushi,hususan ukicheka
  aidha na matamshi,na umbo uloumbika,
  pia na wako ucheshi,wa sura ukiamka
  leo nimepata bahati,nitakueleza muhibu.

  hapa nafunga kitabu,kuendelea sitoweza,
  ila mahaba na tabu,ndwele husoza,
  na dawa muhibu,yenye kunipoza,
  ni yako tabibu, ambayo yaweza
  leo nimepata bahati,nitakueleza muhibu,

  @ DON SHUSHU

 • Michael Bennett
  July 22, 2014 - 7:59 am · Reply

  I just love your (Naubali) poem. I’m absolutely in love with Swahili poems and language. Are you a native Swahili speaker? Please submit or post more poems. I would learn to memorized your poems. You are a very talented and beautiful woman. I pray that I would get a reply from you and your poems. Thank you my Nubian queen.

Leave a Comment