Listen to the poem Nitasimama Mpaka Unipende
Nitasimama,
kima cha urefu wa mbingu,
na nyota zake hewani,
mpaka nisimame wima.
Nitasimama,
kutoka kwenye uoga,
wa niliyemchagua,
lakini akaninyamazisha uhuru wangu.
Nitasimama,
kutoka kivuli,
cha aliyenioa,
lakini akanitia aibu hadharani.
Nitasimama,
kutoka kwenye mapenzi,
ya niliyempenda,
lakini akanilaani kwa mauaji ya halaiki.
Nitasimama,
kutoka kwenye ngao,
za niliyemkimbilia,
lakini akanikabidhi kwenye ulemavu.
Nitasimama,
kutoka mikono michafu,
ya yule niliyemuamini,
lakini akanibaka bila huruma.
Nitasimama,
kima cha urefu wa utukufu,
na sifa ya utu wangu,
mpaka unipende.
*Shairi hili limehamasishwa na ujumbe wa siku ya Valentine mwaka huu ambayo ni siku wanawake billioni moja duniani tunahamasishwa kusimama, kudansi na kutokomeza ukiukaji dhidi ya wanawake.
Nicely writen. lakini kwa kusoma umesema (lakini akaninyamazisha) ila umeandika.. Sasa sijui kama ni typing mistake au ulimean kitu kingine. Congrat, it’s lovely.
Nitasimama,
kutoka kwenye uoga,
wa niliyemchagua,
lakini akaninyamiza uhuru wangu.
Halima asante my dear ni typo kwenye uandishi. Mafua yamenikaba hata screen naona chenga. Sahihi ni “akaninyamazisha”. Remain blessed!
Love the poem! Happy Valentines!
Thank you Aggie. Happy St. Valentine’s Day to you and your dear ones!
Asante kwa shairi zuri sana, ila katika Kiswahili mashairi ya masivina hayana mvuto sana japo yanavutia. Hebu jaribu kutunga ya kimapokeo uone jinsi yanavyovutia kwa utamu wa lugha na mnato wa sauti. All in all hongera sana.
Asante Eric. Nimeandika pia ya namna nyingine ila sijayaweka hapa. Inshallah mungu akijalia nitatoa kitabu chenye baadhi ya mashairi uliyoshauri.